Kiswahili

Mwito wa Tamko la Wanawake wa Sera za dawa za Kimataifa ambazo ni Msaada kwa Wanawake, Watoto, na Familia

Kwenye tukio la Kikao cha Mkutano wa pamoja wa Umoja wa Mataifa kuhusu Madawa, mashirika kutoka duniani kote yanayofanya kazi kuelekea usawa wa kijinsia yamehusisha jumuia ya kimataifa kukamilisha sera ya adhabu kuhusu madawa yanayotishia haki, afya, na usawa wa wanawake, watoto, na familia.

Zaidi ya miaka hamsini baada ya jumuiya ya kimataifa kupitisha Mkataba Mmoja kuhusu Madawa ya Mihadarati, yaitwayo ya kulevya “kumekuwepo na maovu makubwa kwa watu binafsi na “madhara katika jamii na hujuma kwa uchumi wa watu,” uelewa wetu umebaini. Kama inavyotambuliwa na Tume ya Kimataifa kuhusu Sera ya Dawa:

Vita vya kimataifa juu ya dawa za kulevya vimeshindwa, na kumekuwa na madhara makubwa kwa watu binafsi na jamii duniani kote. . . . mageuzi ya kimsingi katika sera za kitaifa na kimataifa za kudhibiti madawa ya kulevya yanatakiwa haraka.

Sera za kudhibiti madawa ya kulevya zenye adhabu zimeangusha hasa wanawake na familia. Utawala wa sasa wa kimataifa wa kudhibiti madawa ya kulevya unahalalisha sharia na matendo ambayo yanawanyima wanawake mamlaka, na yanakiuka kanuni na maadili ya kimsingi kwa usawa wa wanawake.

Tunatambua kwamba:

 • Kuelekeza mawazo kwenye adhabu haijapunguza matumizi ya madawa wala kukomesha biashara ya madawa. Badala yake, udhibiti na matokeo ya sera za kutoa adhabu hufanya biashara ya madawa kuwa yenye faida zaidi na yenye madharaha zaidi, na imezipatia serikali mamlaka ya kuwagandamiza kwa ukali wanawake ambao seheme ya uchumi wao ni katika biashara haramu ya madawa ya kulevya na ambao mara nyingi ni watumiaji au wauzaji wadogo wadogo, ambao mara nyingi husukumwa na haja ya kutafuta riziki kwaajili ya familia zao.
   
 • Kiwango cha dunia nzima cha kufungwa jela kwa wanawake kwa ajili ya makosa madogo yanayohusiana na madawa ya kulevya kinaongezeka katika kiwango cha kutishaMatokeo ya sera za kutoa adhabu kwa madawa ya kulevya yanazidi kuangukia wanawaka, na kiwango cha kufungwa jela wanawake —  hasa ubaguzi wa rangi, ukabila, dini, na kwa uchache mashala ya ngono — inazidi kwa kiwango cha kasi.
   
 • Kufungwa jela kwa wanawake kunawaacha watoto kaika mazingira magumu kwaajili ya kuwatenganisha na mama zao. Idadi kubwa ya wanawake  ambao wamefungwa jela duniani kote kwa ajili ya makosa yanayohusiana na madawa ya kulevya ni wamama wenye watoto. Sera za utekelezaji adhabu  kwa madawa ya kulevya siyo tu zinawanyima wanawake uhuru wao, lakini pia zinahujumu ustawi wa watoto ambao wanalazimishwa kutengwa kutoka kwa mama zao au wanafungwa jela pamoja nao. Inazidi, adhabu kama jibu kwa matumizi ya madawa ya kulevya pia ni pamoja na kuondoa watoto na kusitisha haki za wazazi.
   
 • Wanawake wanapata adhabu isiyo na halali na ambayo si haki kwa ajili ya makosa ya kiwango cha chini cha madawa ya kulevya. Mashirika ya madawa ya kulevya ambayo yanastawi chini ya sera za madawa ya kulevya za kimataifa zilizopo, mara nyingi hujinufaisha na kupata faida kupitia umaskini wa wanawake wenye jukumu la kuhudumia  familia zao, kwa mfano, huwashawishi wanawake kubeba madawa ya kulevya kuvuka mipaka ya kimataifa. Wanawake kisha wako katika mazingira magumu kwa kushtakiwa na kufungwa jela kulingana na uhusiano wao na wengine ambao wanahusika katika biashara ya madawa ya kulevya badala ya uongozi wao wenyewe au mwenendo katika hiyo biashara.
   
 • Kufungwa jela kwa watumiaji wa madawa ya kulevya na wauzaji wadogo wadogo kunatishia usalama wa kiuchumi wa wanawake na familia. Kwa sababu wanawake wana uwezekano zaidi kuwa walezi msingi wa familia, kufanywa mhalifu hujenga mzunguko wa umaskini ambao huzuia wanawake kupata huduma ya afya, maisha na haki za kisiasa na hudhoofisha familia pamoja kijamii na kiuchumi.
   
 • Unyanyapaa na taarifa potovu zinazosasababishwa na sera potovu ya madawa ya kulevya hudhoofisha hali ya wanawake. Sera za madawa ya kulevya za kimataifa zimesababisha kufungwa jela, kuwekwa katika vizuizi vya vituo vya matibabu bila hiari, matibabu ya lazima au uondoaji wa madawa, na kuwekewa vikwazo. Adhabu za aina hiyo bila usawa zinalenga wanawake waliotengwa, hasa wanawake maskini na wanachama wa baadhi ya makabila na vikundi vya rangi. Sera hizi huhamasisha unyanyapaa wa rangi, aibu, na ubaguzi, iwapo au adhabu rasmi zilizowekwa. Wanawake wajawazito na wazazi hasa wananyanyapawa na kampeni za kuongeza chumvi na kueleza visivyo uhusiano wa hatari za madhara kutoka kwa madawa ya kulevya yatokanayo kabla ya kujifungua.
   
 • Wanawake ni rahisi kunyanyaswa na wana maamuzi machache sana wa kupatia utetezi juu huo unyanyasaji na changamoto wakati sera ya kudhibiti dawa ya kulevya inayolenga katika adhabu. Inatambulika duniani kote kwamba unyanyasaji wa kijinsia ni janga lenye upana zaidi, sera za madawa ya kulevya za kimataifa zimeongeza tu haya madhara na kuwaingiza wanawake katika unyanyasaji zaidi. Wanawake wako chini ya ulanguzi, dhuluma na unyanyasaji wa kijinsia  na wale wanaohusika katika biashara ya madawa ya kulevya na wale ambao wanashtakiwa na utekelezaji wa sharia za madawa ya kulevya.
   
 • Kampeni za kutokomeza mimea zinahatarisha afya ya wanawake na watoto. Afua za upande wa usambazaji zimethibitisha kutokuwa na ufanisi katika kuondoa kilimo na uzalishaji wa mihadarati. Badala yake, zinaongeza uharibifu mkubwa wa mazingira. Mazoea ya kutokomeza mimea kama vile unyunyizaji wa madawa husababisha ugonjwa, ikiwa ni pamoja na saratani na madhara ya uzazi, kwa wanawake na watoto ambao hufanya kazi katika maeneo ambayo yana nyunyiza.
   
 • Sera za dawa ya kulevya za kimataifa ambazo husababisha unyanyasaji dhidi ya wanawake na hasara ya maisha zinajenga tabaka la wakimbizi kupitia uhamiaji wa kulazimishwa. Kutokomeza mimea ambako kumeondoa maisha ya watu na unyanyasaji usio na kikomo uliochangiwa na kuzidi kwa sera za kijeshi za kuzuia dawa ya kulevya kumesababisha wanawake kuhama ili kutafuta usalama na fursa. Wakati wanawake wanahama kuvuka mipaka, wanakosa utaifa kabisa na wako hatarini zaidi kwa kunyanyaswa, unyanyasaji wa kimapenzi, kushambuliwa kimwili, kutengwa na watoto wao, na kuwa chini ya mamlaka ya kufukuzwa, kufungwa jela, na adhabu zinginezo kutokana na hali zao.
   
 • Wanawake wanakabiliwa na ubaguzi na hatari ya adhabu katika kutafuta tiba ya dawa madhubuti na sahihi. Wanawake wanakabiliwa na vikwazo kupata dawa ya matibabu sahihi, ikiwa ni pamoja na ukosefu wa huduma ya watoto, ukosefu wa huduma ya habari ya kiwewe, na vitisho vya kukamatwa kama wanaonyesha kwamba wao ni waja wazito. Bila ya kupata huduma ya afya isiyokuwa na ubaguzi, ikiwa ni pamoja na dawa ya matibabu, nafasi ya mwanamke ya kuambukizwa VVU au Mchochota wa ini aina-C, kupitia ukosefu wa makazi, kuzidisha dawa, na kupasuka kwa familia kunaongezeka.
   
 • Wanawake wanaotumia  madawa ya kulevya wanalengwa kwa ajili ya kampeni za uangamizaji na utoaji wa mimba. Unyanyapaa na taarifa ya uongo kuhusu hatari za madhara kutokana na matumizi ya madawa na wanawake wajawazito, uwezo wa uzazi wa wanawake kama hawa, na afya na usalama wa watoto wao hutumika kuhalalisha kuzuia wanawake fulani kutopata mimba au uzazi. Sera ambazo zinaadhibu wanawake ambao ni watumiaji wa madawa wakati wa ujauzito pia huwalazimisha wanawake kutoa mimba kama njia ya kuzuia kukamatwa au kuwekwa kuzuizini.

Kushindwa huku kumekuja kwa gharama kubwa kwa wanawake. Karibu katika kila taifa, sera za madawa za adhabu zina matokeo makubwa kwa wanawake ambao wanakabiliana na umaskini, historia za unyanyasaji wa kimwili na kimapenzi, wasiwasi kutotibiwa afya ya akili, mifumo duni ya msaada, na kubaguliwa kutokana na rangi au kabila. Tunapotazama siku zijazo, tuna nafasi ya kufikiri upya jinsi ya kutibu na kwa ufanisi kuwahudumia wanawake wanaotumia madawa ya kulevya, wauzaji wa madawa, au ni wanaohusishwa na wengine ambao hufanya.

Kwa hivyo tunatoa wito kwa watunga sera ili wadhibiti udhalimu unaosababishwa na kukataza madawa ya kulevya kimataifa na badala yake kuunga mkono sera za madawa zenye msingi katika sayansi, huruma, na haki za kibinadamu na:                                             

 1. Kuchanganya uchambuzi wa kijinsia katika mikataba yote, maazimio, na taarifa juu ya madawa ya kulevya.
 2. Kuweka kupaumbele upunguzaji wa hali za kijamii na kiuchumi zinazochangia ushirika wa madawa wenye matatizo.
 3. Kukaribia matumizi ya madawa yenye matatizo kama suala la afya na kuongeza raslimali kwa hatua ya kuunga mkona afya.
 4. Kuondoa matumizi ya kufungwa jela na adhabu kwa makosa ya madawa ya kulevya. Kufungwa jela kunapaswa kutazamwa kuwa kama kitu adimu na raslimali ghali ambayo inapaswa kutumika tu kwa watu ambao wanasababisha tishio kubwa kwa usalama wa umma na kisha tu kwa kiwango cha kuridhisha cha muda wa kutosha ili kuondoa tishio. Kufungwa jela kwa wanawake ambao ni wajawazito na wenye uzazi kunapaswa kuwa adimu na kwa kipekee
 5. Kuondoa vikwazo vyovyote vinavyosababisha kutiwa hatiani  anbavyo kwamba husababisha athari ya kutoa adhabu ya makosa ya madawa ya kulevya. Hivi vikwazo mara nyingi huongezeka hata zaidi ya hukumu iliyowekwa au adhabu na zaidi kuwabagua wanawake, watoto, na familia.
 6. Kuhakikisha kuwa huduma zote za tiba ya madawa ya kulevya ni msingi wa ushahidi na  kutimiza matibabu maalum ya wanawake, kisaikolojia, na mahitaji ya kijamii, hasa wakati wa ujauzito na uzazi. 
 7. Kufanya utafiti katika athari za sera za kutoa adhabu ya dawa ya kulevya kwa wanawake, watoto, na familia, na kuitumia kuwajulisha na kuboresha utungaji wa sera.
 8. Kuwashirikisha kikamilifu wanawake ambao hutumia madawa ya kulevya katika sera na mipango, utekelezaji na tathmin.